Na Oliver Shayo & John Banda-Dodoma
Mamlaka ya mapato Tanzania [TRA] imewataka wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za Risiti wanazotoa kwa wateja wao ili iwe rahisi kufanyiwa makadirio pindi muda wakutakiwa kulipa kodi unapowadia.
wanapouza bidhaa kutoa risiti ili kutunza kumbukumbu kwani zitawasadia kwenye makadirio ya biashara zao.
Akizungumza na Rasi Fm ofisini kwake Afisa wa kitengo cha Elimu cha TRA Bernabas Masika amesema wafanyabiashara wanapouza bidhaa wanatakiwa kutoa risiti ili kuepuka usumbufu wakati wa makadirio kulingana na viwango vya kodi wanavyotakiwa kulipa.
Masika amesema wafanyabiashara wanapotoa risiti itawasaidia kukadiriwa viwango sahihi vya kodi wanazotakiwa kulipa pamoja na tathimini ya mkadirio ya mwaka.
Amesema ikibainika mfanyabiasha yeyote amekeuka utaratibu wa kutoa risiti atachukuliwa hatua stahiki za kisheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini kulingana na ukubwa wa biashara yake.
Hata hivyo amewataka wanunuzi wa bidhaa wanapokwenda madukani kudai Risiti mara baada ya kufanya manunuzi ya bidhaa yoyote bila ukubwa wala udogo wake.
No comments
Post a Comment