Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » BOMOA BOMOA MANISPAA YA MOROGORO MZIGONI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Manispaa ya Morogoro kwa kushirikiana na mamlaka ya bonde la Wami na Ruvu, wameanza zoezi la ubomoaji wa nyumba zilizojengwa kando kando ya vyanzo vya maji katika safu ya Milima Uluguru.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la mkuu wa mkoa wa Morogoro na kusisitiziwa na Naibu waziri wa ardhi la kuwaondoa wale wote waliojenga ndani ya mita 60 kutoka chanzo cha maji.

Hata hivyo zoezi hilo limeonekana kufanyika kwa kusuasua kutokana na kushindwa kupanda kwa gari linalotumika kwa ajili ya ubomoaji katika milima hiyo, hivyo kupelekea zoezi hilo kufanyika kwa kutumia nyundo na sululu.

Zoezi la ubomoaji wa baadhi ya nyumba zilizojengwa mita 60 kutoka katika vyanzo vya maji kwenye safu ya milima Uluguru, zoezi ambalo limelenga kuweka usalama wa vyanzo hivyo vinavyotegemewa na wakazi waishio mkoani hapa.

Mpaka leo ni nyumba tano tu ambazo zimekwisha bomolewa mpaka sasa, na hii ni kutokana na kujitokeza kwa changamoto ya kushindwa kupanda kwa vifaa vya ubomoaji katika maeneo hayo.

Hata hivyo zoezi hilo limepokelewa kwa hisia tofauti na wakazi waishio katika maeneo haya, huku wakilalamika kutopewa maandalizi ya kutosha kuondoka katika nyumba zao.

Jumla ya Nyumba 125 zimebainika kujengwa katika vyanzo hivyo vya maji, na zote zinatakiwa kubomolewa huku Manispaa hiyo ikisema zoezi hilo ni endelevu na litafuatiwa na wale wote waliojenda kandokando ya barabara.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / BOMOA BOMOA MANISPAA YA MOROGORO MZIGONI

No comments :