Mechi iliyochezwa Uwanjani Nou Camp kati ya miamba ya Soka ya Spain, FC Barcelona na Real Madrid, ikiwa ni pambano la La Liga ambalo Siku zote hubatizwa Jina la El Clasico, ilimazilika kwa Real Madrid kushinda 2-1 na kuimaliza Rekodi ya Mahasimu wao hao wa kutofungwa katika Mechi 39.
Huu ni ushindi wa kwanza katika Mechi yake ya kwanza ya El Clasico kwa Zinedine Zidane kama Meneja.
Hadi Mapumziko Gemu ilikuwa 0-0 na Kipindi cha Pili, Dakika ya 56, Barca walipata Bao kwa Kichwa cha Gerard Pique kufuatia Kona lakini Dakika 6 baadae Real walisawazisha baada ya muvu safi iliyomalizika kwa Karim Benzema kupiga Bao tamu.
Real walifunga Bao Dakika ya 82 kupitia Gareth Bale lakini kwa kushangaza Refa, kufuatia ushauri wa Mshika Kibendera, alilikataa Bao hilo na Sekunde chache baadae Ronaldo aliachia bunduki iliyopiga posti ya juu na kutoka.
Dakika 2 baadae, Real walibaki Mtu 10 baada ya Nahodha wao Serigio Ramos kupewa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Dakika 1 baadae, Cristiano Ronaldo, aliekuwa akizomewa Mechi nzima, aliua Mioyo ya Washabiki wa Nyumbani Nou Camp kwa kupiga Bao la Pili na la ushindi wa 2-1 kwa Real Madrid.
Kabla ya Mechi hii kuanza, Uwanja wa Nou Camp ulifanya heshima maalum kwa Lejendari wao Johan Cruyff aliefariki Wiki iliyopita.
Cruyff alikuwa ni Mchezaji wa Ajax, Barcelona na Timu ya Taifa ya Netherlands ambae pia akaja kuwa Kocha Mkuu wa Barcelona aliewapa Taji la kwanza la Ubingwa wa Ulaya.
Barca bado wanaongoza La Liga wakiwa na Pointi 76 wakifuata Atletico Madrid wenye Pointi 70 na Real wapo wa 3 wakiwa na Pointi 69.
VIKOSI:
Barcelona: Bravo; Alves, Piqué, Mascherano, Alba; Busquets, Rakitic, Iniesta; Messi, Suárez, Neymar
Akiba: Ter Stegen, Sergi Roberto, Bartra, Rafinha, Munir, Turan, Vermaelen
Real Madrid: Navas; Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo; Kroos, Casemiro, Modric; Bale, Benzema, Ronaldo
Akiba: Casilla, Nacho, Rodríguez, Vázquez, Jesé, Isco, Danilo
LA LIGA
kesho Jumapili Machi 20
Ratiba/Matokeo:
>>>Saa za Bongo
Ijumaa Aprili 1
Rayo Vallecano 2 Getafe CF 0
Jumamosi Aprili 2
Atletico de Madrid 5 Real Betis 1
Las Palmas 2 Valencia C.F 1
FC Barcelona 1 Real Madrid CF 2
2305 Celta de Vigo v Deportivo La Coruna
Jumapili Aprili 3
1200 Athletic de Bilbao v Granada CF
1600 Malaga CF v RCD Espanyol
1815 SD Eibar v Villarreal CF
2030 Sevilla FC v Real Sociedad
Jumatatu Aprili 4
2030 Levante v Sporting Gijon
No comments
Post a Comment