LIVERRPOOL na Tottenham Leo zimetoka Sare 1-1 huko Anfield na kutoa mwanya mkubwa kwa Leicester City Kesho Jumapili kupanua pengo lao kileleni katika mbio za Ubingwa wa
Ligi
Kuu England

Matokeo ya Leo yamewaacha Tottemnham Nafasi ya Pili kwenye Ligi wakiwa wamecheza Mechi 1 zaidi ya Vinara Leicester na kuwa Pointi 4 nyuma ya Vinara hao.
Ikiwa Jumapili Leicester, wakiwa kwao King Power Stadium, wataifunga Southampton basi wataselelea kileleni wakiwa Pointi 7 mbele na Mechi zikiwa zimebaki 6 tu.
Hii Leo huko Anfield, Liverpool walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 51 la Phillippe Coutinho na Harry Kane kuisawazishia Spurs katika Dakika ya 63.
VIKOSI:
Liverpool: Mignolet, Clyne, Lovren, Sakho, Moreno, Henderson, Can, Milner, Coutinho, Lallana, Sturridge.
Akiba: Toure, Allen, Origi, Ibe, Skrtel, Smith, Ward.
Tottenham Hotspur: Lloris, Walker, Alderweireld, Wimmer, Rose,
Dier, Dembele, Son, Eriksen, Alli, Kane.
Akiba: Mason, Vorm, Trippier, Chadli, Onomah, Carroll, Davies.
REFA: Jon Moss
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumapili Aprili 3
1530 Leicester v Southampton
1800 Man United v Everton
Jumamosi Aprili 9
1445 West Ham v Arsenal
1700 Aston Villa v Bournemouth
1700 Crystal Palace v Norwich
1700 Southampton v Newcastle
1700 Swansea v Chelsea
1700 Watford v Everton
2030 Man City v West Brom
Jumapili Aprili 10
Jumapili Aprili 10
1530 Sunderland v Leicester
1800 Liverpool v Stoke
1800 Tottenham v Man United
Jumatano Aprili 13
2200 Crystal Palace v Everton
No comments
Post a Comment