Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » MKUU WA IDARA YA UTUMISHI HALMASHAURI KIKAANGONI JIJINI MWANZA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amemueleza Mkuu wa Idara ya Utumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Sigrifid Kaunala kuwa ni miongoni mwa watumishi watakaochunguzwa kutokana na kugundulika kuwepo kwa baadhi ya watumishi hewa waliopata mamilioni ya fedha kama mikopo kutoka taasisi za fedha.

Mongella alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Jiji hilo ambao pamoja na mambo mengine alitumia nafasi hiyo kuzungumzia suala la watumishi hewa.

Alisema baada ya uchunguzi wa uhakiki wa awamu ya pili wa watumishi hewa uliofanywa na Serikali mkoani humo umebaini kuwepo kwa watumishi watano (majina yao yanahifadhiwa) waliojipatia mikopo ya mamilioni ya fedha kutoka taasisi za fedha hali inayoonesha baadhi ya mikopo hiyo isingetolewa bila ya kibali cha waajiri wao.

“Mkuu wa utumishi nasikia hata wewe unahusika kwenye sakata hili la watumishi hewa, haiwezekani mambo haya yatokee na wewe usijue na wewe ni miongoni mwa watu tunaowachunguza,” alisema Mongella.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa ya kuhakiki watumishi hewa, Waryoba Sanya alisema kazi ya kuhakiki watumishi walioko kazini lilianza jana kwa kuanza na uhakiki wa watumishi wote wa Ofisi Kuu ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza walioko kazini na kuwa lilikuwa linaendelea vizuri.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / MKUU WA IDARA YA UTUMISHI HALMASHAURI KIKAANGONI JIJINI MWANZA

No comments :