Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » WATOTO WA MKOANI DODOMA WAITAKA SERIKALI KUONGEZA WAWEKEZAJI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Na Peter Mkwavila,DODOMA.
WATOTO wa mkoa wa Dodoma wameiomba serikali ya mkoa kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje katika kipindi hiki ambacho serikali imeamua kuhamishia makao yake hapa kwa upande wa sekta ya huduma za jamii ikiwemo ya kiafya na kielimu ili kukidhi mahitaji ya ongezeko la watu linalotarajiwa.

Ombi hilo lilitolewa mbele ya mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mndeme,kwenye tamasha la watoto hao lililofanyika jana wakati walipokuwa wakisoma risala yao.

Akisoma risala hiyo kwa niaba ya watoto wezake Jacob Siogopi alisema kuwa mkoa wa Dodoma hivi karibuni utaanza kupokea wageni mbalimbali wa serikali ikiwa ni matokeo ya utekelezaji wa awamu ya tano ya uamuzi wa kuhamia.

“Hivyo mkuu wa wilaya sisi kama watoto wa Dodoma tukependa wageni wakifika hapa wasijutie uamuzi wa serikali kuhamishia makao makuu yake hapa kwetu na wakifika wakute mazingira safi na huduma bora za kijamii ikiwepo ya kielimu na kiafya”alisema.

Aidha watoto hao wameitaka serikali kuhakikisha katika kipindi hiki cha kuhamishia makao makuu hayo,kutenga na kuyaendeleza maeneo ya kutosha kwa ajili ya michezo na burudani ya watoto ikiwa na kuhamasisha na kuwasaidia wawekezaji wanaokusudia kuwekeza katika huduma mbalimbali ya watoto.

Pia wazazi na walezi wamekumbushwa kuwa kutumia fursa ya uwekezaji katika huduma za watoto hasa katika suala la elimu kwa kuwa ni sehemu ya kiuchumi kwa mkoa huu wa Dodoma kama wataendelezwa zaidi kielimu.

Alisema kuwa watoto ni sehemu ya serikali wasipoandaliwa vema kwa malezi bora wanaweza kuwa mzigo na hasara kwa familia na taifa kwa kuwa watakuwa wamepoteza nguvu kazi hivyo tunatakiwa kupatiwa malezi stahiki ambayo yatakuwa faida kwao.

Naye Mkurugenzi wa Pilipili Event Emmanuel Mathias aliwataka wazazi na walezi kuwasaidia watoto wao wanaojitokeza kuwa na vipaji kwa kuwatengenezea kwa lengo la kuwaendeleza zaidi badala ya kuwazuia.

Mathias alisema kuwa wazazi na walezi wanao wajibu mkubwa wa kukuza vipaji vya watoto hao kwa kuwa ni moja ya sehemu ya kujipatia ajira ambayo inayoweza hata na kukuza uchumi wa Taifa hili kwa kupitia vipaji vyao.

“Hakuna haja ya kumkanya kwa mtoto anayeibuka na kipaji kinachotakiwa kumsaidia na kumtengenezea ajira hiyo ya badaye ambayo itakayo mwezesha kujitengemea na kuondokana na utegemezi kwa wazazi na walezi wake”alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mndeme alisema kuwa serikali kama haitakubari kuona maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya watoto yakichukuwali na kuvamiwa na ujenzi holela unaofanywa na baadhi ya wananchi.

“Hivyo wale wote waliovamia na watakaovamia maeneo hayo ambayo yametengwa kwa ajili ya viwanja vya michezo watanyanganywa na kuchukuliwa hatua za kisheria na kamwe hawatafumbiwa macho kwa kuonewa huruma kwa suala kama hilo”alisema.
Mwisho

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / WATOTO WA MKOANI DODOMA WAITAKA SERIKALI KUONGEZA WAWEKEZAJI

No comments :