Wapiganaji wa Kikurdi wamefanikiwa kuingia mji wa Sinjar kaskazini mwa Iraq, siku moja baada yao
kuanza operesheni ya kuutwaa kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State (IS).
Operesheni hiyo ilisaidia na mashambulio ya angani kutoka kwa ndege za muungano unaoongozwa na Marekani.
Hayo yakijiri, jeshi la Iraq linasema limeanzisha operesheni ya kuuokomboa mji wa Ramadi magharibi mwa nchi hiyo ambao ulikuwa umetekwa na wapiganaji wa IS.
Kuuokomboa mji wa Sinjar kutaziba mawasiliano kati ya ngome mbili za IS Raqqa na Mosul.
Mji huo ulipotekwa na IS mwaka jana, mamia ya maelfu ya watu wa dini ya Yazidi walikwamba baada ya kutorokea mji wa Sinjar.
Mamia ya wanaume waliuawa na wanawake wa Yazidi wakatekwa na kutumiwa kama watumwa wa ngono.
Shambulio hilo la Sinjar lilikuwa moja ya sababu zilizoifanya Marekani kuanza mashambulizi ya angani kusambaratisha ngome za IS nchini Iraq, baada ya kuibuka kwa wasiwasi wa kutekelezwa kwa mauaji ya halaiki.
Marekani baadaye ilipanua mashambulio yake hadi Syria mwezi uliofuata.
No comments
Post a Comment