Rais wa Senegal Macky Sall amesema
hazina ya $1.9bn (£1.2bn) iliyoundwa na mataifa ya Ulaya ni hatua nzuri lakini akasema pesa hizo hazitoshi.
Viongozi hao wamesema lengo lao ni kukabiliana na mizizi ya tatizo la wahamiaji.
Mkutano huo uliitishwa baada ya wahamiaji 800 kufa maji meli yao ilipozama baharini baada ya kuondoka Libya.
Rais Sall, ambaye kwa sasa anaongoza muungano wa mataifa ya Afrika Magharibi, aliambia wanahabari pembezoni mwa mkutano huo kwamba pesa hizo zilizoahidiwa “hazitoshi bara lote la Afrika”.
Lakini baadaye, akizungumza katika kikao na wanahabari alisema amefurahishwa na hazina hiyo, lakini akasema angependa kuona pesa zaidi zikitolewa.
Rais wa Niger Mahamadou Issoufou alikariri matamshi ya kiongozi huyo wa Senegal na akaongeza kuwa uongozi wa ulimwengu unafaa kufanyiwa mageuzi, na biashara duniani ifanywe kuwa ya haki zaidi.
Rais wa Baraza la EU Donald Tusk amesema mkutano huo uliofanyika Malta umekubalia kuhusu “orodha ndefu ya hatua zitakazotekelezwa kufikia mwisho wa 2016”.
No comments
Post a Comment