Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » NIMEKUWEKEA MKUSANYIKO WA HABARI ZA KIMATAIFA HAPA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

MALI
Wanajeshi wameingia katika hoteli ya Radisson Blu mjini Bamako baada ya watu wenye silaha kuishambulia na kushikilia watu mateka.

Uvamizi huo wa wanamgambo hao ulitekelezwa asubuhi kwenye hoteli hiyo ya kifahari ambayo hupendwa sana na raia wa mataifa ya nje.

Ripoti za karibuni zaidi zinasema mateka 80 wameokolewa kutoka kwenye hoteli hiyo ambayo inamilikiwa na Wamarekani.

Awali, kampuni inayomiliki hoteli hiyo Rezidor Hotel Group ilikuwa imesema watu 170 walikuwa wameshikiliwa mateka na "watu wawili".

Baadhi ya ripoti zinasema watu walioshambulia hoteli hiyo huenda wakafika 10.

Milio ya risasi inasikika kutoka nje ya hoteli hiyo yenye vyumba 190, shirika la habari la AFP linasema.

Ufaransa ambayo imekuwa na wanajeshi Mali tangu 2013 inaripotiwa kutuma wanajeshi wake kusaidiana na wanajeshi wa Mali. Aidha, polisi maalum wapatao 50 wametumwa kutoka Paris.

Rais wa Mali aliyekuwa ziarani Chad amekatiza safari yake na anatarajiwa kurejea Mali wakati wowote.
Agosti, wapiganaji wa Kiislamu waliua watu 13, wakiwemo wafanyakazi watano wa UN, baada ya kushikilia mateka watu katika mji wa Sevare, katikati mwa Mali.

Ubalozi wa Marekani mjini Bamako umeandika kwenye Twitter kwamba unafahamu kuhusu shambulio hilo na kuwashauri wafanyakazi wake pahala salama nao raia wawasiliane na familia.

NIGERIA

Kundi la Boko Haram limefanya mashambulizi dhidi ya kambi ya kijeshi, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Shirika la habari la Xinhua limezinukuu duru za usalama wa Nigeria zikisema leo kuwa, wanamgambo wa Boko Haram wameshambulia kambi ya kijeshi iliyoko katika mji wa Gudunbali, kwenye jimbo la Borno ambalo lilikuwa ngome ya kundi hilo. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanajeshi 107 wa Nigeria hawajulikani walipo.

Msemaji wa jeshi la Nigeria, Sani Kukasheka Usman amethibitisha kutokea shambulio hilo lakini hakusema lolote kuhusu hasara zilizosababishwa na shambulio hilo.

Duru za usalama za Nigeria zimesema pia kuwa, kundi la Boko Haram limeteka kifaru aina ya T-72 kwenye shambulizi hilo.

Kundi la Boko Haram lilianzisha mashambulizi yake mwaka 2009 nchini Nigeria na hadi hivi sasa watu wasiopungua 17 elfu wameshauawa na zaidi ya milioni mbili la laki tano wengine, wamekuwa wakimbizi.

LIBERIA
Maafisa wa afya wa Umoja wa Mataifa wanasema kumetokea maambukizi mapya ya Ebola nchini Liberia chini ya miezi mitatu baada ya nchi hiyo kutangazwa kutokuwa na ugonjwa huo.

Mgonjwa wa sasa ni mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka kumi kutoka viungani mwa mji wa, Monrovia.

Wachambuzi wanasema habari hii ni pigo kubwa kwa nchi ya Liberia ambayo imeshuhudia zaidi ya maambukizi elfu kumi na vifo zaidi ya elfu nne tangu ugonjwa wa Ebola kugunduliwa nchini humo.

UTURUKI

Uturuki imewaonya raia wake kuhusiana na kutembelea Misri hususan katika rasi ya Sinai.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki leo imetoa tamko na kuwaonya raia wake kuhusu kutembelea Misri hususan katika rasi ya Sinai na kusisitiza kuwa, raia wa Uturuki wenye nia ya kutembelea eneo la Sinai wanapaswa kujua kuwa kuna hatari ya kukumbwa na lolote lile katika eneo hilo.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, safari kadhaa za ndege za Uturuki kuelekea rasi ya Sinai nchini Misri, zimefutwa.

Ni hivi karibuni tu ambapo ndege ya abiria ya Russia iliripuliwa kwa bomu huko Sinai Misri. Kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuhusika na shambulio hilo.

Kwa upande wake Misri inasema kuwa, hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kuwa, kuangaka ndege ya abiria ya Russia katika anga ya Sinai kumetokana na shambulio la kigaidi.

CZECH

Waziri Mkuu wa Czech amesema kuwa, makundi ya kigaidi yanatumia nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kupitishia watu wao barani humo.

Shirika la habari la Ufaransa limemnukuu Bohuslav Sobotka akisema hayo jana na kuongeza kuwa, mashirika ya kijasusi yamethibitisha kwamba makundi ya kigaidi yanatuma wanachama wao barani Ulaya kupitia nchini Czech.

Sobotka ameongeza kuwa, Czech si nchi pekee inayotumiwa na makundi ya kigaidi kujipenyeza barani Ulaya.

Waziri Mkuu huyo wa Czech ameongeza kuwa, hakuna uchunguzi mkubwa wanaofanyiwa watu wanaoingia barani Ulaya na suala hilo limeyarahisishia makundi ya kigaidi kupenyeza watu wao barani humo.

Itakumbukwa kuwa, gaidi mmoja aliyetiwa mbaroni nchini Ufaransa mwezi Agosti mwaka huu alikiri kuwa aliamrishwa atumie njia ya Czech kuingia barani Ulaya.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / NIMEKUWEKEA MKUSANYIKO WA HABARI ZA KIMATAIFA HAPA

No comments :