Mtandao wa WhatsApp umekamata sana
sasahivi kutokana na watu wengi kupendelea kuutumia mtandao huo,
inakuwaje una smartphone yako alafu unazuiwa kutumia WhatsApp ?!! Brazil
imewakuta hiyo.
Ishu ilianza hivi, Mahakama ya Brazil
iliagiza wamiliki wa mtandao huo kuwapa nafasi ya kuweza kuingilia na
kupekua taarifa za kila mtumiaji wa mtandao wa WhatsApp aliyepo Brazil,
lakini wamiliki hao hawakuwa tayari kuingia masuala ya mawasiliano ya
mtu binafsi, wakapingana na maagizo hayo.
agizo likatolewa na Mahakama
kwamba mtandao huo ufungwe kwa saa 48, maana yake ni kwamba watu wote wa
Brazil kuanzia jana hawakuwa na mawasiliano ya WhatsApp.
Lakini baadae, Zuckerberg alipost pia ujumbe kwenye ukurasa wake Facebook kushukuru baada ya watumiaji wa WhatsApp kurudishwa tena hewani.
No comments
Post a Comment