Wananchi wa Rwanda jana walijitokeza kwa wingi kwenye kura ya maoni
kuhusu mabadiliko ya Katiba na kupasisha kwa asilimia kubwa marekebisho
hayo yaliyolalamikiwa vikali na Umoja wa Ulaya na wanaharakati wa
kupigania demokrasia na makabidhiano salama ya madaraka.
Gazeti la serikali la The New Times limeandika leo kuwa, asilimia 98.1 ya wapiga kura wamepigia "Yego" yaani Ndio, marekebisho hayo.
Matokeo ya awali yaliyotangazwa jana usiku na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Rwanda NEC kutoka wilaya 21 kati ya wili 30 zilizoshiriki kwenye kura hiyo ya maoni yanaonesha kuwa marekebisho hayo yamepitishwa kwa asilimia 70 suala ambalo linabashiri kupitishwa kwa zaidi ya asilimia 98 marekebisho hayo.
Hata hivyo Rais Paul Kagame hadi hivi sasa hajaamua iwapo ataendelea kugombea urais au la. Toleo la mtandaoni la gazeti la New Vision la nchini Uganda limemnukuu Rais Paul Kagame wa Rwanda akisema kuwa, atatangaza uamuzi wake baada ya matokeo rasmi ya kura hiyo ya maoni.
Gazeti hilo pia limemnukuu Kagame akisema kuwa, hana mpango wa kuwa rais wa maisha wa Rwanda.

No comments
Post a Comment