Muda wa Kocha Dylan Kerr kuinoa Simba umefikia mwisho baada ya uongozi kwa pamoja kukubaliana kuachana naye rasmi.
Uongozi
wa Simba umefikia uamuzi wa kuachana na Kerr baada ya kutoridhishwa na
mwenendo wa kikosi hicho katika Ligi Kuu Bara na baadaye Kombe la
Mapinduzi lililomalizika hivi karibuni mjini Zanzibar.
Pamoja
na kutokuwa na matokeo mazuri lakini inaonekana uongozi haujaridhishwa
na uchezaji wa kikosi cha timu hiyo na mambo yalikuwa mabaya zaidi
katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar.
“Kweli kamati ya utendaji imefanya kikao cha muda cha dharura na kukubaliana na hilo,” kilieleza chanzo kutoka Zanzibar.
“Taarifa
tulizonazo ni kwamba kocha Kerr ameitwa Dar es Salaam ambako ataondoka
kesho Jumanne akiwa Dar es Salaam ataelezwa kuhusiana na uamuzi huo wa
uongozi kumtupia virago na nafasi yake atapewa Kocha Majanja ambaye juzi
aliingia mkataba kama kocha msaidizi.”
Chanzo kilipoulizwa kama uongozi hauwezi kubadili uamuzi hiyo kesho, kilieleza:
"Tunaamini
hakuna nafasi hiyo, hata Kerr mwenyewe ameishashitukia, atakuwa anajua
kwamba mambo yatakuwa hivyo. Usiku huu ameamua kutoka kwenda kuiaga
Zanzibar (kicheko)."
Taarifa
nyingine zimeeleza kwamba Kerr raia wa Uingereza ameponzwa na ubishi na
uongozi umekuwa ukimlaumu kutofanya kazi kwa kujituma.
Wakati
fulani, Rais wa Simba, Evans Aveva aliwahi kujitokeza mazoezini
kimyakimya wakati Simba ikijifua kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu Dar es
Salaam (UDSM), hali iliyoonyesha wazi uongozi hauridhiki na utendaji wa
Mwingereza huyo aliyechukua nafasi ya Goran Kopunovic aliyeondoka baada
ya kutaka dau la Sh milioni 100 ili aongeze mkataba mpya Simba.
Kerr
anaondoka na kuiacha Simba katika nafasi ya tatu baada ya mechi 13 na
imekusanya pointi 27 nyuma ya Yanga yenye 33 na Azam FC kileleni ikiwa
na 35.
Mwingereza
huyo anaiacha Simba ikiwa imeshinda mechi 8, sare 3 na kupoteza mbili,
imefunga mabao 20 ikishika nafasi ya tatu kwa ufungaji baada ya Yanga
yenye 30 na Azam FC yenye 27 huku ikiwa imeruhusu mabao 9, ikiwa safu
bora ya ulinzi katika nafasi ya nne baada ya Azam iliyoruhusu mabao 8,
Mtibwa Sugar mabao 7 na Yanga yenye safu ngumu zaidi imefungwa mabao
matano tu.
Simba inaanchana ana Kerr leo lakini taarifa zinaeleza, Mkenya huyo naye anaweza kuunganishwa na Kerr.
“Tayari
wote wamepanda boti wanakwenda Dar es Salaam ambako watakutana na
uongozi. Baada ya hapo, kitakachofuata hatujui,” kilieleza chanzo.
“Lakini taarifa zinasema wote wawili safari imewakuta, sasa ni suala la kusubiri nafikiri hadi mchana.
Iddi Salim amewahi kuwa kocha wa makipa wa Gor Mahia, pia timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars.
No comments
Post a Comment