Njombe
MADEREVA wa pikipiki wanao fanya biashara ya usafirishaji
maarufu Bodaboda mkoani Njombe wameiomba serikali kuwasaidia
kuwaparuhusa ya kuingia ndani ya stendi ya mkoa huo baada ya kuzuiliwa
kuingia humo.
Inadaiwa na bodaboda hao kuwa wanazuiliwa kuingia katika
stendi hiyo na kukamatwa wanapo egesha pikipiki zao nje ya stendi hiyo
na kuwa huwa wanatozwa faini pindi wanapo kuwa wameendesha nje ya stendi
na wanapo ingia ndani.
Wakitoa malalamiko yao kwa mbunge wa mkoa wa njombe viti
maalumu kupitia Chadema Lusia Mlowe madereva hao wamesema kuwa serikali
inavyo fanya hiyo inawanyima uhuru wateja wao.
Philimoni Edward, Mwenyekiti bodaboda, mkoa wa Njombe, (2)
Franco Mhoha Katibu wa madereva bodaboda mkoa wa njombe Albeto Danda
dereva bodaboda wanaeleza
Hata hivyo mbunge huyo akizungumza na madereva hao na
kuchukua kelo zao alisema kuwa anaiomba halmashauri kuwaruhusu bodaboda
kuingia stendi na abilia wao ili kuto wanyanyasa abilia na madereva.
Mbunge huyo yupo katika ziara ya mkoa mzima ili kujua
changamoto za wananchi mbalimbali katika mkoa huo tayari kwa
kuziwasilisha bungeni mapema mwaka huu.
Na Furaha Eliab via John Banda,
No comments
Post a Comment