Njombe
ZAIDI ya heka 20 za mahindi za wakazi wa kijiji cha Mpanga
halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe zimefyekwa na watu
wanaodaiwa ni askari wa wanyamapoli wa hifadhi ya bonde la mto Balali maeneo ya
Mpanga Kipengele.
Wakizungumza kwa masikitika katika mashamba hayo wananchi wa
kijiji hicho wamesikitishwa na kindo hicho kwa kuwa eneo hilo
wanalima baada ya kuhamishwa katika kiji cha Mpanga na kuhamia eneo hilo ambalo kwa sasa
linaitwa Mpanga mpya.
Mzee Barton Mbuchi na Mwenyekiti wa mfreji huo Lusundo
Lusupo wanaeleza
Wananchi hao wamesema kuwa mbali na kulipia pia wafyekaji
hao wamekuja katika eneo hilo
ikiwa ni mara ya pili na kufanya uharibifu wa mahindi, Migomba ambayo thamani
yake inakadiliwa kuwa haizidi milioni 30 huku ndizi lizizo komaa wakiondoka
nazo.
Hata kuvyo Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Njombe Lucia Mlowe
amefika katika eneo hilo na kutoa pole kwa waathilika wa kukatiwa mahindi na
kusema kuwa serikali ni vema inefanya mazungumzo na wananchi hao na kufikia
muafaka kuliko ilivyo fanya.
Aidha meneja wa Tanapa hifadhi ya kipengele alisema kuwa yeye sio msemaji na kutaka kuwasiliana na Wizara kwa ufafanuzi.
Na Furaha Eliab,via John Banda
No comments
Post a Comment