Katika mkutano huo uliofanyika muda mfupi uliopita Cristiano Ronaldo alipata nafasi ya kumzungumzia mpinzani wake Lionel Messi baada ya kuulizwa anamzungumziaje muargentina huyo, Ronaldo alijibu:‘Ningekuwa na uwezo Ronaldo ningependa niupate mguu wake wa kushoto, mguu wake huo una uwezo kuliko wa kwangu,’ alijibu CR7 na baadae Neymar nae akamuunga mkono kwa kusema yeye angependa awe na miguu yote miwili ya mchezaji mwenzie wa FC Barcelona.
Katika upande mwingine Ronaldo alizungumzia skendo ya rushwa katika soka na akasema: ‘Ninachoweza kusema ningependa rushwa isiwepo, sio tu kwenye soka bali katika mfumo mzima wa kimaisha vilevile.’
ZILIVYOKUWA KURA ZA Ballon d'Or
Lionel Messi 41.33%
Cristiano Ronaldo 27.76%
Neymar 7.86%
No comments
Post a Comment