Na Denis kazenzele
Wakati vijana wanaangaika wapi watapata ajira kumbe kuna vijana wanatumia fursa moja kuweza kujikwamua kwa njia ya pili kupitia ya kwanza, hii inakuja iwapo vijana kwa umoja wao watajiingiza katika miradi mbalimbali na kuwahusisha wanaoifahamu vizuri miradi husika na aina ya watu wanaotaka kujiungamanisha nao{kuandamana nao katika miradi husika}
hii imeonekana hata kwa hawa jamaa ambao wao ni wasanii na wajasiriamali wa kikundi cha KIGURU SANAA GROUP kinachopatikana maeneo ya dodoma makulu hapa hapa mkoani dodoma ambao wao wapo na kikundi hiki kwa jina hilo la uigizaji na sanaa nyinginezo lakini pia ili kujikimu wameamua kujiingiza katika shughuli za kilimo,ufugaji,uzalishaji wa vipaji vya aina tofauti n.k.
Pia januari 14 mwaka huu Alhamis ya wiki ijayo wanazindua movie yao {bongo movie }yenye asili ya kitanzania inayokwenda kwa jina la KIDOLE CHA TITI, Hivyo usisahau kupata nakala yako kama mchangiajiukuaji kwa sanaa ya kitanzania na kusaidia kwa njia moja au nyingine suala la upatikanaji wa ajira kwa vijana wa kitanzania.
{Ukiachana na idadi yao kuwa ni zaidi ya wanachama ishirini lakini viongozi wa juu ni Sospeter Mwaluko {director na msemaji wa kikundi}, Rajab Yasin {Mwenyekiti },Jasmin Iddi { Matron wa kikundi} na Geofrey Hamis {Mtendaji wa kikundi}.
Je sisi vijana tuliobaki kulia lia juu ya ajira tunafanya nini zaidi ya kuamka na kupambana? na vipi serikali kupitia wizara za vijana,sanaa pia wizara inayojishughulisha na ajira mnawaona vijana hawa na mnajifikiria nini juu ya kujituma kwao?
Tazama Picha kibao wakiwa Studio za RASI FM RADIO ..DODOMA Tanzania wakitoa muongozo,mafanikio na matarajio yao ya baadae .
Sospeter Mwaluko director wa Kiguru Sanaa Group {mwenye shti jeupe} akizungumza jambo ndani ya Sayari mpya ya Rasi Fm Radio |
Sospeter Mwaluko director wa Kiguru Sanaa Group {mwenye shti jeupe} akizungumza jambo ndani ya Sayari mpya ya Rasi Fm Radio
matron wa Kiguru sanaa group Jasmin Iddi akiongea juu ya mafanikio ya kikundi hicho |
Sospeter Mwaluko director wa Kiguru Sanaa Group {mwenye shti jeupe} akizungumza jambo ndani ya Sayari mpya ya Rasi Fm Radio
kushoto ni matron wa kiguru sanaa group Jasmin Idd na kulia ni Rajab Yasin Mwenyekiti wa kiguru sanaa group |
mtangazaji wa Rasi Fm Radio Hamis Shaaban {pistol} akiuliza swali kwa wanasanaa wa kiguru |
kiongozi wa watu wenye jamii ya Albino{walemavu wa ngozi} michael salali akiwapa ushauri wanasanaa wa Kiguru Sanaa Group ndani ya studio za rasi fm radio jana jumamosi |
No comments
Post a Comment