Najua headlines kwa sasa ni stori za mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Aly Samatta kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi ya ndani ya Afrika.
Baada ya tuzo kumalizika, Samatta alilala
Lakini imenifikia list ya waliomuwezesha Samatta kutwaa tuzo hiyo na kuwashinda golikipa TP Mazembe Robert Mutebe Kidiaba wa Kongo na Baghdad Bounedjahmualgeria anayeichezea klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia. Kama ulikuwa hujui tuzo hiyo upigiwa kura na makocha wa timu za taifa, ila baada ya utolewaji wa tuzo kumalizika shirikisho la soka la Afrika CAF lilitoa list kamili ya makocha waliompigia kura Samatta.
via millard ayo
No comments
Post a Comment