MKUU wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma
Bituni Msangi amesema utamaduni wa
wananchi kujisaidia vichakani umepungua na hivyo kupunguza idadi ya wanaougua
magonjwa yanayotokana na uchafu.
Alitoa kauli hiyo juzi katika hotuba yake
iliyosomwa kwa niaba yake na Ofisa
Tarafa Wilaya ya Kongwa Denis Semindu wakati wa kusherehekea mafanikio ya
kufikia utimilifu wa Usafi wa mazingira katika kijiji Ugogoni yenye kauli mbiu Mazingira
Safi yasiyokuwa na kinyesi.
Alisema kabla ya mradi wa Usafi wa
Mazingira Tanzania (UMATA) kuanza wananchi wengi wa Wilaya hiyo walikuwa hawana
vyoo na hivyo kujisaidia kwenye vyoo vya majirani au kwenye vichaka,porini, hivyo
kufanya uchafuzi mkubwa katika vyanzo
vya maji na mazingira kwa ujumla.
"Hali hiyo ilichangia kwa kiasi
kikubwa magonjwa ya kuharisha, kipindupindu
na yale yanayotokana na maji machafu" alisema.
alisema kabla ya Mradi huu wa UMATA kijiji cha Ugogoni
hakikuwa kwenye hali nzuri ya usafi wa mazingira licha ya kufanyiwa
uhamasishaji wa mara kwa mara.
Alisema kutokana na takwimu zilizokusanywa
na kamati mnamo tarehe Oktoba 30, 2015 Kijiji kilikuwa na takribani kaya 229,
ambapo kati ya kaya hizi ni kaya 11 tu hazikuwa na vyoo na kaya 61 tu ndizo
zilikuwa na vifaa vya kunawia mikono (kibuyu chirizi).
Pia alisema mpaka kufikia Desemba 20, 2015
kijiji kilikuwa na asilimia 100 ya kaya zote kuwa na kutumia vyoo, uwepo wa
vifaa vya kunawia mikono baada ya kutoka chooni, mashimo ya taka na vibuyu
chirizi
Akisoma risala ya Shirika la SAWA, Asnat
Charles alisema shirika hilo linahusika
na uhamasishaji wa ujenzi na matumizi ya vyoo bora na kuchochea mabadiliko ya
tabia za usafi katika jamii na shuleni kwa kutumia mbinu ya kushirikishi.
Pia Mradi umejikita kutoa elimu ya afya na
usafi wa mazingira kwa shule za msingi ikimlenga mtotoambaye ndiye chachu ya
mabadiliko kwa mtoto mwenzake, ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.
Ofisa Afya Kata ya Ugogoni, Iqubal Janja
alisema mila na desturi zilisababisha watu wengi wasiwe na vyoo na kujisaidia
vichakani na magonjwa yaliyotokana na uchafu yalikuwa mengi.
Mwandishi: John Banda
Mhariri: Denis J. Kazenzele
Tarehe: march 03.2016
No comments
Post a Comment