picha haihusiana na habari |
Elimu bure kwa sasa ndio wimbo upendwao na wengi wananchi wa kitanzania, lakini pia wasomi na wanaosema walichosikia wametoa changamoto lukuki juu ya elimu bure sasa moja kati ya changamoto hizo ipo katika shule ya sekondarI Nzuguni B Mjini dodoma.
Walimu na wanafunzi wa
shule ya msingi Nzuguni B wanaishi kwa
kumwomba Mungu ili awanusuru na magonjwa ya mlipuko kutokana na tundu moja la
choo kutumiwa na wanafunzi zaidi ya mia mbili huku walimu wa shule hiyo
wakikosa vyoo.
Akizungumza
kwa masikitika mwalimu mkuu wa shule
hiyo Liliani Luiva amesema wameamua kuishi kwa kumwomba Mungu kutokana na idadi
hiyo ya wanafunzi kujisaidia kwenye tundu moja la choo huku wakikanyaga
vinyesi vya wenzao na kisha kwenda
madarasani na viatu vilevile vilivyokanyaga vinyesi na kukaa
chini kwa idadi hiyo hiyo ya wanafunzi.
Amesema ongezeko la
idadi hiyo ya wanafunzi iliyotokana na mwitikio mkubwa wa wazazi kuwaandikisha watoto wengi kutokana na mwito
wa serikali wa elimu bure huku kukiwa hakuna ongezeko la miundombinu ye yote ikiwemo
vyoo.
Aidha
mwalimu huyo amesema mazingira ya shule hiyo sio rafiki kwa kufundishia wanafunzi kutokana na shule hiyo kukosa uzio.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Joseph Masinga amesema wanafunzi hao wanasoma katika
mazingira hatarishi kutokana na mwingiliano wa watu unaotokana na eneo la shule
hiyo kutopimwa hivyo kukosa hati miliki hali inayosababisha wenyeji kujenga
mpaka karibu na maeneo ya shule hiyo.
Mwandishi: Lydia Kishia na John Banda
Mhariri: Denis J. Kazenzele
Tarehe: march 03.2016
No comments
Post a Comment