Waziri wa zamani wa sheria wa Ufaransa ametoa wito wa kuwekwa wazi uhakika na ukweli kuhusu mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi yaliyotokea Rwanda mwaka 1994.
Christiane Taubira ambaye ametoa heshima kwa wahanga zaidi ya laki nane waliouawa mwaka 1994 nchini Rwanda, amesema leo kuwa uhakika wa mauaji hayo ya kimbari unapaswa kuwekwa wazi. Vilevile ametaka kuwekwa wazi habari zote zinazotabakishwa kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda.
Rwanda inasema kuwa serikali ya wakati huo ya Ufaransa ilishirikiana na watawala wa Kihutu wa Rwanda kutekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa kabila la Watutsi.
Hadi sasa watu kadhaa walioongoza mauaji ya kimbari ya Rwanda wametia nguvuni na kuhukumiwa katika mahakama maalumu iliyokuwa mjini Arusha nchini Tanzania.
Karibu watu milioni moja wengi wao wakiwa Watusti waliuawa katika mauaji hayo ya kimbari yaliyofanywa na Wahutu wenye misimamo mikali.
Credit: Iribswahili
No comments
Post a Comment