Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw. Elius Mwakalinga akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu kutekelezwa kwa mpango wa Serikali wa kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanapata makazi bora ambapo wakala huo unajenga nyumba 10,000 ili kutimiza azma hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Milki Bw. Baltazar Kimangano na kushoto ni Mkurugenzi wa Ushauri Bw. Edwin Nnunduma.
Mhandisi Ujenzi kitengo cha Upimaji na Ukaguzi Majengo toka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakwanza kulia Bi Khadija Salum akionesha kwa waandishi wa Habari sehemu ya vifaa vilivyonunuliwa na wakala huo kwa ajili ya kupima ubora wa majengo yaliyokwisha jengwa na yale yanayoendelea kujengwa ili kuhakikisha kuwa Serikali inakuwa na majengo yenye ubora kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa.
Habari
Serikali kupitia wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imenunua vifaa vya kupima Ubora wa Majengo bila kuyaharibu (Non destructive Testing equipments) .
Hayo yamesemwa Leo Jijini Dar es salaam na Mtendaji Mkuu waTBA Bw. Elius Mwakalinga wakati wa mkutano na vyombo vya Habari uliolenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa na wakala huo.
Akifafanua Mwakalinga amesema kuwa wakala huo umenunua vifaa vya kisasa ili kuwezesha ukaguzi wa ubora wa Majengo ya Serikali ili kuwa na majengo yenye Ubora unaotakiwa.
“Lengo la kununua vifaa hivi ni kuhakikisha kuwa majengo yote ya Serikali yanakuwa na ubora kwa kuwa tutayapima yaliyopo na yale yanayojengwa ili tuweze kuchukua hatua pale inapodi” alisisitiza Mwakalinga.
Akieleza umuhimu wa vifaa hivyo Mwakalinga amesema kuwa hakutakuwa na wasiwasi tena kuhusu uwezekano wa wakandarasi kudanganya wakati wa ujenzi.
Aidha vifaa hivyo vitawezesha Wakala kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika majengo ya Serikali ili kubaini hali ya ubora wa majengo hayo ambapo gharama ndogo za ada ya ushauri zitatozwa kwa Taasisi husika.
Vifaa hivi ni kama Rebund hammer inayotumika kupima uimara wa zege iliyokauka, cover meter kwa ajili ya kupima ukubwa wa nondo na umbali uliowekwa.
Akitaja vifaa vingine Mwakalinga amesema kuwa ni “Utrasonic system/testing device” kwa ajili ya kupima muonekano wa ndani ya zege iliyokauka.
Mbali ya jukumu la kuhakiki ubora wa majengo ya Serikali, Wakala umeendelea na mpango wa ujenzi wa nyumba zinazouzwa kwa gharama nafuu kwa watumishi wa umma ambapo mpango wa wakala huo ni kujenga nyumba elfu kumi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
No comments
Post a Comment