Siku moja baada ya kumtimua kocha wake Peter Maes klabu ya KRC Genk ya Mbwana Samatta hatimaye imevunja mwiko kwa kuifumua AA Gent jumla ya magoli 2-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji uliochezwa kwenye uwanja wa Cristal Arena mjini Genk.
Genk walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 19 kupitia kwa kiungo mshambuliji AlejandroPozuelo baada ya kupata goli hilo wenyeji hawakubweteka waliendelea kulishambulia lango la wageni kama nyuki mnamo dakika ya 26 mshambuliaji mwenye uchu wa kufumania nyavu Raia wa Ugiriki Nikolaos Karelis kufunga la pili baada ya kinda Leon Bailey kuangushwa ndani ya 18.
Hadi mapumziko Genk walikwenda wakiwa mbele kwa magoli hayo mawili na kipindi cha pili kilianza kwa timu zote mbili kufanya mabadiliko ambayo hayakuweza kuisaidia Gent katika dakika ya 53 wenyeji walipata pigo baada ya Nikolaos Karelis kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Mbwana Samatta.
Mpaka mpira unamalizika wenyeji wameibuka na ushindi wa jumla ya magoli 2-0 na kwa matokeo hayo wamebaki kwenye nafasi ya 9 wakiwa na alama 28 huku wakiwa wamefunga magoli 25 na kufungwa 30.
No comments
Post a Comment