Bado siku mbili mwaka 2016 umalizike tuingie mwaka 2017 kuna mambo mengi ya kukumbuka kwa mwaka 2016, moja kati ya hayo ni hii list ya majina maarufu katika jezi ya wachezaji wa Ligi Kuu England kwa mwaka 2016.
Mtandao wa Sportdirect.com umetaja majina ya wachezaji 10 ambao majina yao yamekuwa maarufu katika jezi kwa mwaka 2016, kwa maana nyingine jezi zenye majina yao ndio zimetawala mitaani kwa mwaka 2016.
Staa wa Man United aliyeweka rekodi ya usajili ya dunia Paul Pogba ndio kinara katika list hii, akifuatiwa na nyota mwenzake wa Man United Zlatan Ibrahimovic, jumla ya majina manne ya wachezaji wa Man United yameingia katika TOP 10 hii.
1- Paul Pogba (Man United)
2- Zlatan Ibrahimovic (Man United)
3- Alex Sanchez (Arsenal)
4- Mesut Ozil (Arsenal)
5- Phillipe Coutinho (Liverpool)
6- David de Gea (Man United)
7- Sadio Mane (Liverpool)
8- Dimitri Payet (West Ham United)
9- Eden Hazard (Chelsea)
10- Marcus Rashford (Man United)
No comments
Post a Comment