Inawezekana wewe ukawa ni moja kati ya watu wanaomfuatilia sana staa wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, basi taarifa ikufikie kuwa timu ya FC Barcelona ambayo imemlea na kumkuza kisoka imetoa TBT picha zake na video na inawezekana ukawa hujawahi kuziona.
Lionel Messi alizaliwa June 24 1987 Rosario Argentina ni mtoto wa tatu katika familia ya watoto wa nne ya mzee Jorge Messi ambaye alikuwa ni meneja katika kiwanda cha chuma, wakati mama yake Celia Cuccittini alikuwa akifanya kibarua katika kiwanda cha utengenezaji wa sumaku.
Lionel Messi akiwa na miaka mitano alijiunga na timu ya mtaani ya Club Grandoli iliyokuwa inafundishwa na baba yake, ambayo alidumu nayo hadi akiwa na miaka sita akahamia Newell’s Old Boys, timu hiyo katika kipindi cha miaka minne walipoteza mchezo mmoja kitendo kilichofanya wapewe jina la utani kuwa “The Machine of 87′ ikiwa ni mwaka aliyozaliwa.
Messi akiwa na umri wa miaka 11 alipatwa na tatizo la ukuaji kutokana na homoni zake kutokuwa sawa, kitu ambacho kilifanya timu yake ya utotoni kushindwa kumlipia gharama za matibabu, ndio mkurugenzi wa FC Barcelona wa wakati huo Carles Rexach akasema atagharamia matibabu yake ila kama atakubali kuhamia Hispania.
Credit: Millardayo.com
No comments
Post a Comment