Mwanamke moja raia wa New Zealand amefariki katika visiwa vya Caribbean baada upepo mkalia kutoka kwa injini ya ndege kumuangusha chini.
Kisa hicho kilitokea katika uwanja maarufu wa Princess Juliana ambao uko umbali wa mita chache kutoka baharini.
Watu wanaostarehe kwenye ufukwe wanaweza kutembea hadi kwa ua wa uwanja wa ndege kutazama ndege zikipaa.
Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo wa umri wa miaka 57, alikuwa akishikilia ua wa uwanja wa ndege kabla ya upepo mkali kutoka kwa injni ya ndege kumrusha nyuma na kusababisha apate majeraha. mabaya.
- Alipelekwa hospitalini kwa matibabu lakini akafariki baadaye.
Eneo hilo ni maarufu kwa watalii kwa sababu ndege hupita chini zaidi kabla ya kutua kwenye uwanja wa ndege ulio karibu.
Bara ya nde imeanzia umbali wa mita 50 tu kutoka kwa ua na katika umbali sawa na maji ya bahari.
No comments
Post a Comment