Ligi Daraja
la Kwanza (StarTimes League) inaendelea wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa
katika viwanja mbalimbali, huku timu 3 za juu kutoka katika kila kundi zikipata
nafasi ya kupanda Ligi Kuu msimu ujao moja moja.
Kundi A, Jumamosi Mji Mkuu watawakabili
Africa Lyon uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, KMC dhidi ya Kiluvya uwanja wa
Mabatini Mlandizi, Polisi Dodoma watacheza dhidi ya Friends Rangers uwanja
wa Mgambo Mpwapwa, huku Jumapili Polisi Dar wakiwakaribisha Ashanti
uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Kundi B, Njombe Mji watakua wenyeji wa
Kimondo uwanja wa Amani Njombe, Lipuli FC dhidi ya Kurugenzi uwanja wa Wambi –
Mafinga, uwanaj wa Majimaji mjini Songea JKT Mlale watakua wenyeji wa Polisi
Morogoro, huku Jumapili kukichezwa mchezo mmoja Ruvu Shooting dhidi ya
Burkinafaso uwanja wa Mabatini, Mlandizi.
Kundi C, Rhino Rangers watawakaribisha
JKT Kanembwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora, Panone FC dhidi ya Geita Gold
uwanja wa Ushirika mjini Moshi, uwanja wa Karume Musoma, wenyeji Polisi Mara
watacheza dhidi ya Polisi Tabora, huku siku ya Jumapili Mbao FC wakiwakaribisha
JKT Oljoro uwanja wa CCM Kirumba
No comments
Post a Comment