Baada ya kuwatimua kazi wa Hispania matajiri wa jiji la Dar es salaam Azam FC wameendelea kufanya siri kubwa katika kumpata mrithi wa Hispanyol, kuna taarifa kocha wa zamani wa TP Mazembe, Lamine N’Diaye, naye anaweza kutua Chamazi.
N’Diaye raia wa Senegal ambaye aliwahi kukipiga katika kikosi cha Cannes ya Ufaransa, ni kati ya makocha wanaopewa nafasi ya kuinoa Azam FC.
“Kweli kuna ishu ya Kali (Ongala). Anaweza kuanza kazi na timu halafu wakikubaliana na N’Diaye, basi anakuja kuwa bosi.
“Unajua ni kocha mkubwa, Mazembe amekuwa hadi mkurugenzi wa ufundi. Ni mtu mtaalamu sana na soka la Afrika, usisahau aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Senegal,” kilieleza chanzo.
N’Diaye aliisaidia Mazembe kuchukua makombe ya ubingwa wa Congo na makombe mengine, ubingwa wa Afrika kuanzia akiwa kocha na baadaye mkurugenzi wa ufundi kwani jana mchana Azam FC ilitangaza kumtimua Kocha Zeben Hernandez na makocha wasaidizi wote.
N’Diaye alitua TP Mazembe mwaka 2010, baadaye mwaka 2013 akawa mkurugenzi wa ufundi. Lakini amewahi kufundisha timu ya taifa ya Senegal na Kabla aliifundisha Coton Sport ya Cameroon kwa mafanikio pia Maghreb Fez ya Morocco.
No comments
Post a Comment