Imebainika kuwa, baadhi ya raia wa Kiafrika wanaopigwa mnada katika magendo ya binadamu nchini Libya wananyofolewa viungo vyao vya mwili na kuuzwa.
Amebainisha kuwa: "Ukweli wa mambo ni kuwa, baadhi ya raia hao wa Afrika hawauzwi kwa ajili ya kwenda kufanya kazi Ulaya, bali kwa ajili ya biashara ya viungo vya binadamu kama maini na mapafu."
Wakili huyo na mtetezi wa haki za binadamu ameongeza kuwa, wahajiri hao waliojikuta kwenye mtego wa magendo ya binadamu wanapewa dawa za kulala na kisha viungo vyao vinachukuliwa."
Wahajiri wa Afrika wanaouzwa kama bidhaa nchini Libya |
Hivi karibuni, televisheni ya CNN ilirusha hewani mubashara mnada wa kuuza Waafrika huko nchini Libya ambapo kila mtu alikuwa akiuzwa kwa dola zisizopungua 400 za Kimarekani.
Duru mbali mbali za kimataifa, ukiwemo Umoja wa Afrika na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zimekosoa vikali biashara hiyo ya utumwa mambo leo inayofanyika nchini Libya.
No comments
Post a Comment